All for Joomla All for Webmasters

Speeches

HOTUBA YA BI. SICILY KARIUKI, CBS, WAZIRI WA HUDUMA ZA UMMA, VIJANA NA JINSIA WAKATI WA SHEREHE ZA KUKABIDHIWA KWA HUNDI YA HAZINA KUBORESHA KIUCHUMI MNAMO JUMATATU TAREHE, 25 APRILI 2016 KATIKA TRANSNATIONAL SACCO HALL, ENEO BUNGE LA CHUKA/IGAMBANGOMBE.

Katibu Mkuu, Maswala ya Jinsia,
Halmashauri za Wenyeviti na Wakurugenzi,
Kaimu Afisa Wakuu wa, (Uwezo Fund, YEDF and WEF)
Wageni Waalikwa
Mabibi na Mabwana


Ni furaha yangu kuungana nanyi wakati wa sherehe za kutolewa kwa hundi kutoka kwa hazina ya Uboreshaji Kiuchumi na Ufahamishaji hapa eneo bunge la Chuka/Igambangombe

Mabibi na Mabwana,
Changa moto kuu zinazo wakabili Kina mama, Vijana na Walemavu ni zito na zina hitilifiana. Kina Mama na Vijana wanakabiliwa na uhaba wa pesa za kuanzisha biashara, kutokuwa na ujuziwa kibiashara na dhana mbovu. Hii imepunguza nafasi zao za kupata mikopo kuanzisha au kustawisha biashara zao.

Vijana na Wanawake ni zaidi ya aslimia sitini ya idadi ya watu nchini, lakini licha ya idadi kubwa yao, ni kana kwamba hawatiliwi maanani katika ustawi wa kiuchumi na kijamii nchini.

Kuwawezesha kiuchumi makundi haya ni moja ya ajenda kuu ya serikali ya Jublilee inayo wajibikia kupitia kwa kubuni Hazina ya Uwezo, Hazina ya Ustawi wa Kibiashara ya Vijana na Wanawake miongoni mwa juhudi nyingine sawa na hizo.

Ni dhamira ya serikali kupitia kwa Hazina hizi kuwapa mikopo Wakenya ili kustawisha mawazo yao ya biashara hivyo basi kujiajiri wenyewe na kuimarisha hali ya maisha yao.

Mabibi na Mabwana
Hazina ya Uwezo imebuniwa muafaka kuongeza utoaji wa ufadhili katika kuimarisha biashara za vijana, kina mama na walemavu katika kiwango cha maeneo bunge hivyo basi kusaidia kuafikia Ruwaza ya Maendeleo ifikapo mwaka wa 2030.
Hazina hizo tatu zilizoko chini ya usimamizi ya Wizara yangu zinatoa mafunzo na mwelekeo kuwawezesha wanaohusika kunufaika na agizo la serikaliyakutengaaslimia 30 ya huduma na biashara za serikali kupitia mpango wake wa kuwezesha kiuchumi.

Mabibi na Mabwana,
Hazina ya Uwezo
Ni furaha yangu kuwajulisha kwamba kufikia sasa Hazina ya Uwezo imegawanya jumla ya shilingi za Kenya bilioni tano nukta 35 katika maeneo yote ya uwakilishi bungeni mia mbili na tisini.
Kati ya pesa hizo, shilingi bilioni nne nukta 82 zimeidhinishwa kupewa makundi elfu arubaini na tisa, mia tisa thelathini na nane kote nchini wenye wanachama binafsi wapatao elfu mia nane na moja, mia nanesabininamoja.
Kaunti ya Tharaka Nithi iligawiwa jumla ya shilingi xxxxxxxxx za hazina ya Uwezo wakati wa kipindi cha matumizi ya pesa za serikali cha mwaka wa 2014/2015 na kugawiwa makundi xxxxxxx yenye wanachama binafsi wapatao XXXXXXXX

Hivyo basi, Eneo bunge la Chuka/Igambang’ombe lilipokea shilingi XXXXXXXXXXXX zikiwa za hazinaya uwezo katika kipindi hicho na kugawanyiwa makundi xxxxxxx yenye wanachama binafsi wapatao XXXXXXX.

Hazina ya Kufadhili Kina mama-WEF
Hazina hii ya kufadhili kina mama imegawa shilingi bilioni saba nukta 51 kwa makundi yapatao elfu hamsini na tisa, mia nane ishirini na nne yenye watu binafsi wapatao milioni moja, elfu mia moja sitini na saba, mia tatu kumi na saba kote nchini tangu ilipobuniwa. Kaunti ya TharakaNithi imepokea shilingi milioni hamsini na tatu, elfu mia tatu sitini na sita na mia tisa na mbili ambazo zimegawiwa makundi mia nne thelathini na saba yenye wanachama binafsi wapatao elfu saba na arobaini na tatu tangu ibuniwe.
Hazina hiyo imetoa LPO za udhamini wa shilingi milioni kumi na tano, elfu mia saba themanini na tatu, mia tano ishirini kwa wateja hamsini tangu kuanzishwa kwa mpango huo mpya mwezi wa Agosti mwaka uliopita.
Hazina hiyo husaidia katika utoaji wa thamana za bondi na kubuniwa kwa Vyama vya ushirika vya SACCO.

Hazina ya Ustawi wa Kibiashara kwa Vijana-YEDF
Hazina hii ya kuwafadhili biashara za vijana kufikia sasa imegawa shilingi bilioni kumi na moja nukta nne kwa makundi elfu hamsini na moja, mia mbili thelathini na tano kuwanufaisha wanachama binafsi wapatao elfu mia nane arobaini, mia saba ishirini na saba.
Kaunti ya TharakaNithi imepokea shilingi milioni mia moja sabini na nane , elfu themanini na nane, mia tatu hamsini na saba ambazo zimegawiwa vijana elfu ishieini na tatu mia saba tisini na sita. Eneo bunge la Chuka/IgambaNg’ombe limepokea milioni arobaini na tano,elfu mia tano tisini na nane,mia saba arobaini na nne kuwanfufaisha vijana elfu tano mia tatu ishirini na tano.
Hazina hiyo pia inatoa LPO za kiwango cha shilingi milioni ishirini.

Mabibi na Mabwana,
Nachukua fursa hii kutambua wajibu bora unaotekelezwa na hazina hizi tatu za kuboresha maisha nikisema ipo haja ya kuzidhibiti kwa hali na mali kwa lengo la kuwahudumia Vijana, wanawake na Walemavu.
Ni kiwa Waziri anayesimamia Mpango wa Kuwezesha Kiuchumi vijana na wanawake, nakariri kujitolea kwangu kuhakikisha Wakenya zaidi wanapata ufadhili kutoka kwa serikali ili kuwawezesha kutumia kikamilifu uwezo wao hivyo basi kupiga jeki ustawi wa kiuchumi wa taifa hili.
Nikitamatisha, natoa wito kwa walionufaika wote na mikopo hii kutoka kwa serikali kuilipa kwa wakati ufaao ili kuwawezesha wakenya zaidi kunufaika kwayo.
Na kwa ushauri huu, ni furaha yangu kuwatunuku hundi hizi kwa wahusika.


Ahsanteni Sana

Our Partners

WEF Awards